Sekunde Quotes

Quotes tagged as "sekunde" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Akili yangu itakaponipeleka kwa mgonjwa hospitalini halafu sekunde hiyohiyo jicho langu likacheza au kiungo changu chochote cha mwili kikauma na kuacha ghafla ‘bila’ sababu yoyote, najua kile ninachokifikiria kuhusu mgonjwa huyo ama kitatokea au hakitatokea. Nikifikiria amepona, halafu ghafla kichwa kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake. Yaani, hatapona. Nikifikiria amekufa, halafu ghafla kichwa au kiungo kingine chochote kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake pia. Yaani, hatakufa. Hivyo, nikifikiria amepona, nikifikiria amekufa, na kichwa kikaniuma na kuacha, sekunde hiyohiyo natakiwa kumwombea mgonjwa huyo. Kama ni kupona, apone kama Mungu alivyokusudia; na kama ni kufa, afe kama Mungu alivyokusudia. Si kama Shetani alivyokusudia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Siri ya mafanikio yako ni chumba chako. Dali linasema anga ndicho kipimo cha kufikiria; Dirisha linasema utazame nje uone fursa zilizopo ulimwenguni; Feni linasema uwe mtulivu usikurupuke kufanya lolote; Kalenda inasema uwe mtu anayekwenda na wakati; Kioo kinasema ujitazame na ujiamini kabla ya kutenda lolote; Kitabu cha dini kinasema unapaswa kumwamini Mungu ili uishi; Kitanda kinasema ujifunze kuwa na likizo; Mlango unasema usipitwe na fursa ya aina yoyote ile hapa duniani; Saa inasema kila sekunde ina thamani sana katika maisha yako hivyo tumia muda wako vizuri. Amka uishi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ndani ya chumba, akiwa bado amechanganyikiwa, akiwa hajui Debbie alikokwenda, Murphy alisikia walinzi wakipiga kelele nje. Kamanda huwa anakuwa shetani nyakati kama hizo. Alibeba pumzi. Mikononi mwake akiwa na M-16, Debbie kichwani; Murphy alishangaza umati wa watu! Risasi zaidi ya sitini zilifyatuka katika bunduki, mlango wote ukabomoka – ndani ya sekunde kumi!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa makini, nadhani, utapata maana ya ujumbe unaopewa na Roho Mtakatifu kwa wale wanaomwamini Mungu au ‘daemon’ (tofauti na ‘demon’) kwa wale wasiomwamini Mungu. Mimi, kwa mfano, huwa najali muda. Jicho langu likicheza au kiungo changu chochote cha mwili kikiuma ghafla na kuacha, au hata kisipoacha, jambo lolote ninalolifikiria muda huo ambapo jicho linacheza au kiungo changu cha mwili kinauma najua ni ujumbe kutoka kwa Mungu na una uhusiano na jambo hilo ninaloliwaza. Hivyo, kuanzia sekunde hiyo napaswa kuwa makini sana na jambo lolote ninalolifikiria.”
Enock Maregesi