UKUBWA NA UDOGO
KAWAIDA UKUBWA UDOGO
Mtu Jitu Kijitu
Mto Jito Kijito
Mti Jiti Kiguu
Mguu Guu Kiguu
Nyumba Jumba Kijumba
Ndege Dege Kidege
Mkoba Koba kikoba
Mbuzi Buzi Kibuzi
Ndovu Dovu Kidovu
Ndoo Doo Kidoo
Kichwa Jichwa Kijichwa
Njia Jia Kijia
Mlango Lango Kilango
Mwizi Jizi Kijizi
Nguruwe Guruwe Kiguruwe
Mtoto Toto Kitoto
Mdudu Dudu Kidudu
Ngozi Gozi Kigozi
Ngoma Goma Kigoma
Kivuli Jivuli Kijivu
Mbwa Jibwa Kijibwa
Kikapu Jikapu Kijikapu
Mzee Zee Kizee
Uso Juso kijuso
Mkate Kate Kikate
Mke Jike Kijike
Msichana Sichana Kisichana
Kitabu Jitabu Kijitabu
Mvulana Vulana Kivulana
Kipande Jipande Kijipande
Udongo Dongo Kidongo
Mwanamke Janajike Kijanajike
Kinywa Jinywa Kijinywa
Mji Jiji Kijiji
Moyo Joyo Kijoyo
Kidole Jidole kijidole
Moto Joto Kijoto
Mfupa Fupa Kifupa
Mlima Lima Kilima
Ndama Dama Kidama
Kiatu Jiatu Kijiatu
Kikombe Jikombe Kijikombe
Ng’ombe Gombe Kigombe
Chungu Jungu Kijungu
Mwanamwali Janajali Kijanajali
Mkono Kono Kikono
sahani Jisahani kijisahani
Zoezi
Fuata maagizo
1. Mbwa mweusi alikimbia (badili katika ukubwa)
2. Moyo wa mtu ulidunda (badili katika udogo)
3. Mtoto yule ni mdogo (badili kwa wingi katika
ukubwa)
4. Kichwa cha ndovu ni kizito (badili katika
ukubwa)
5. Kijoka kilichouma gombe ni hiki (badili katika
wingi)
Majina ambata
Majina haya ni maneno mawili
yanayoambatanishwa pamoja na kutamkwa
kama jina moja rasmi.
1. Kiamshakinywa breakfast
2. Mwanamaji a sailor
3. Kifunguamimba a first born child
4. Njugumawe ground nuts
5. Mwendawazimu a mad person
6. Pimamaji a water/ spirit level
7. Kinasasauti a microphone
8. Batamzinga a turkey
9. Kionjamchuzi beards
10. Mjamzito a pregnant woman
11. Mkaajikoni a person who likes
staying at home
12. Kinukamto a restless person
13. Mwanamwali a maid
14. Mwanasiasa a politician
15. Mwanamji a town dweller
16. Mchanjakuni a person who splits
firewood
17. Mwanyumba a name of people who
married from the same family
18. Dondadungu persistent ulcer
19. Njiapanda crossroads
20. Kitindamimba a last born child
21. Mlariba a money lender
22. Askarikanzu a policeman who does
not put on uniform
23. Kidagatonge epiglottis
24. Mkemwenza a co-wife
25. Kirukanjia a prostitute
26. Mwanasheria a lawyer
27. Mwananchi a country man
28. Mwanahewa a pilot
29. Mfanyibiashara a business man/woman
30. Mwekahazina a treasurer
31. Kichwamaji a stubborn person
32. Njugunyasa a type of nuts.
33. Mwanaserere a doll
34. Mwanariadha an athlete
35. Mwanamchezo a sportsman/ woman
36. Mwanajeshi an army man/ woman
37. Bwanaharusi the bridegroom
38. Biarusi the bride
39. Mwanagwenzi an apprentice
40. Kiinimacho a magic trick
41. Mwanakondoo a lamb
42. Mwanambuzi a kid
43. Mpitanjia a passersby
44. Mwanadamu a human being