Nenda kwa yaliyomo

Ala ya muziki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Ala za muziki za Kiafrika, katika makumbusho ya Museum of Natural History, Washington, D.C., Marekani.

Ala ya muziki ni kifaa kinachotoa sauti zinazotumiwa katika muziki. Kila ala ya muziki inatoa mitetemo katika hewa inayoendelea kusambaa na kupokewa na masikio kama sauti.

Kimsingi kila kitu kinachotoa sauti kinaweza kutumiwa kama ala ya muziki, lakini kwa kawaida jina hili linatumika kwa vitu vilivyotengenezwa hasa kwa shabaha hii. Wakati mwingine hata sauti ya binadamu inatajwa kama ala ya muziki.

Kuna aina nyingi za ala za muziki. Mara nyingi zinaainishwa na kutajwa kutokana na mbinu zake za kutoa sauti:

  • ala za mitemo (kwa Kiingereza idiophone) ambako ala yote inatetema, kama vile kengele, mafurungu, marimba
  • ala za nyuzi (ing. chordophone) kama vile gitaa, fidla, selo, zeze au piano; hapa uzi au waya iliyokazwa inapigwa au kuchuliwa hivyo inaanza kutetema
  • ala za utando (ing. membranophone) kama vile ngoma, tari, hapa utando inatoa mitetemo ikipigwa
  • ala za hewa (ing. aerophone) ambako nguzo ya hewa inatetemewa, mfano filimbi, kinanda cha filimbi, zumari, kipenga, baragumu, au tarumbeta. Katika kundi hili hewa inaweza kupititishwa kwenye kona kali kama kwa filimbi, au kwa kipande cha tete inayotetema katika mwendo wa hewa, au kwa kutumia midomo kama asili ya mitetemo kama kwenye tarumbeta.
  • katika karne ya 20 zilibuniwa ala za muziki elektroniki ambazo zinatoa sauti kupitia kipaza sauti.

Wengine hutofautisha ala za muziki kutokana na namna ya matumizi, kama vile kupiga, kupuliza hewa, kupiga vibanzi au funguo (keyboard), kuchulia waya.

Kila jamii na kila utamaduni kwenye dunia imewahi kubuni ala zake za pekee.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ala ya muziki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.