Embriolojia
Makala hii, au sehemu za makala hii, inahitaji vyanzo au marejeo yoyote. Tafadhali saidia kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo vya kuaminika. Habari zisizowekewa vyanzo zinaweza kuwekewa alama na kuondolewa. (Julai 2007) |
Embriolojia (kutoka Kigiriki ἔμβρυον, embryon, "hajazaliwa, kiinitete" na λογία -logia elimu, taaluma) ni sayansi inayojishughulisha na ukuaji wa kiinitete kutoka kwa utungisho wa yai kukua hadi kipindi cha kijusi.
Baada ya utengano, seli zinazojigawanya ziitwazo morula, zinakuwa tufe shimo au blastula, kinachomoka kitundu kwa upande mmoja.
Katika wanyama wenye pande mbili zinazofanana, blastula inakua katika moja ya njia mbili. Jinsi blastula inavyokua inatumika kupanga ufalme mzima wa wanyama katika vipande viwili (tazama: Asili ya kiembriolojia ya mdomo na mkundu). Kama kitundu cha kwanza (blastopore) kinakuwa mdomo, mnyama huitwa protostome, kikiwa mkundu, mnyama huitwa deuterostome. Hakina protostome wanazingatia wingi wa wanyama wanaokosa uti wa mgongo, kama vile wadudu, minyoo, na konokono, wakati hakina deuterostome ndio kodata au wanyama wenye uti wa mgongo kwa mfano binadamu, ndege, na samaki. Baada ya kipindi, lazima blastula ijitofautishe ili iwe na muundo mbalimbali zaidi uitwao gastrula.
Gastrula yenye blastopore yake inajipanga kwenye rusu tatu za chembe hai (rusu vyanzo) ambazo zinaunga viungo vyote mwili pamoja na tishu:
- Rusu ya ndani (inayopakana na mashimo ya blastula), inayoitwa endoderimu, ndiyo chanzo cha vyombo vya mmeng'enyo, mapafu, na kibofu cha mkojo.
- Rusu ya katikati, inayoitwa mesoderimu, inaunga misuli, mifupa na mfumo wa damu.
- Rusu ya nje, inayoitwa ectoderimu, inakuwa mfumo wa neva na ngozi.
Kwa binadamu, neno "kiinitete" linahusu tufe ya chembe hai zinazojigawanya (zaigoti) kutoka wakati wa kujiingiza ukuta wa tumbo la kizazi (uterasi) wa mpaka mwisho wa wiki nane baada ya kutungwa. Zaidi ya wiki ya nane, kinitete kinakuwa kinaitwa kijusi. Viinitete vya spishi nyingi vinafanana katika hatua za ukuaji za mwanzo kwa sababu spishi hizo zina asili moja ya mabadiliko. Milingano hiyo kwenye spishi huitwa miundo homalagasi ambayo ni miundo yenye kutenda kazi moja na utaratibu mmoja ama inayofanana utendaji kazi na utaratibu kwa kuwa spishi zenye miundo hiyo zimetofautiana kutoka asili moja.
Historia
Hivi karibuni kama karne ya 18, wazo lililoongeza katika embriologia liliitwa muundo wa kwanza kwa sababu watu walidhani mtoto mchanga mdogo kabisa anaitwa "homunkulus" alikuwa amekwishaumbwa kabisa kwenye shahawa. Wazo hilo linasema mtoto huyu anakuwa mkubwa wakati yumo kwenye tumbo la kizazi. maelezo ya shindano la maendeleo ya kiinitete liliitwa epigenesisi na lilielezeka mapema miaka 2,000 na Aristotle. Wazo hilo la epigenesisi, umbo la mnyama linakua hatua kwa hatua kutoka yai linalokosa umbo maalum. Kama somo la hadumini liliboreka wakati wa karne ya 19, wasomi wa viumbe hai waliona viinitete vikikua hatua hadi hatua na wakapendelea maelezo yale la Aristotle yaani epigenesisi.
Kwenye kundi la waanzilishi wa embriologia ya kisasa wamo Gavin de Beer, Charles Darwin, Ernst Haeckel, J.B.S. Haldane, na Joseph Needham, wakati embriologia ya msingi sana ilitoka katika kazi ya Aristotle na wasomi wakubwa wa viungo vya ndani wa kiitaliano: Aldrovandi, Aranzio, Leonardo da Vinci, Marcello Malpighi, Gabriele Falloppia , Girolamo Cardano, Emilio Parisano, Fortunio Liceti, Stefano Lorenzini, Spallanzani, Enrico Sertoli, Mauro Rusconi, nk [1] Wengine wachangiaji muhimu ni William Harvey, Kaspar Friedrich Wolff, Heinz Christian Pander, Karl Ernst von Baer, na Agosti Weismann.
Baada ya miaka ya 1950, waligundua muundo wa helikali wa DNA pamoja na kuongezeka ujuzi katika somo la baiolojia, maendeleo yalijitokeza kama shamba la utafiti kwenye malengo matatu: la kwanza kugundua mahusiano kati ya vinasaba na mabadiliko ya kiumbo, la pili kuamua ni kinasaba gani kinachosababisha kila badiliko la kiinitete, na la tatu kuelewa jinsi hivyo vinasaba vinarekebishwa.
Embriologia ya wanyama wenye uti wa mgongo na wasio na uti wa mgongo
Kanuni nyingi za embriologia zinahusu wanyama wasio na uti wa mgongo pamoja na wale wenye uti wa mgongo. [2] Kwa hiyo, somo la embriologia ya wasio na uti wa mgongo limesogeza mbele somo la embriologia ya wenye uti wa mgongo. Hata hivyo, kuna tofauti pia. Kwa mfano, aina mbalimbali ya wasio na uti wa mgongo wanatolea viluwiluwi kabla havijakamilika maendeleo kamili; katika mwisho wa kipindi cha kiluwiluwi, mdudu kwa mara ya kwanza anafanana na mdudu mzima yuko sawa na mzazi au wazazi wake. Embriologia ya wasio na uti wa mgongo yenyewe inatofautiana kati ya aina moja ya mdudu kwenda nyingine. Kwa mfano, wakati buibui wanatamia wakiwa wazima wadudu wengi hukua kwa kupitia hata kipindi kimoja cha kiluwiluwi.
Utafiti wa embriolojia wa kisasa
Hivi sasa, embriolojia imekuwa ni muhimu kwa ajili ya utafiti wa udhibiti wa vinasaba kwa utaratibu wa kimaendeleo (kwa mfano morphogeni), uhusiano wake na ishara za seli, umuhimu wake kwa ajili ya utafiti wa magonjwa fulani na wa mabadiliko ya vinasaba na uhusiano wake na utafiti wa seli shina.
Tanbihi
- ↑ [4] ^ Massimo De Felici, Gregorio Siracus, The rise of embryology in Italy: from the Renaissance to the early 20th Century, Archived 5 Januari 2010 at the Wayback Machine. Int. J. Dev. Biol. 44: 515-521 (2000).
- ↑ Parker, Sybil. "Invertebrate Embryology," McGraw-Hill Encyclopedia of Science & Technology (McGraw-Hill 1997).
Marejeo
- Embryology - History of embryology as a science. " Science Encyclopedia. Web. 6 Nov 2009. <http://science.jrank.org/pages/2452/Embryology.html>.
- "Germ layer." Encyclopædia Britannica. 2009. Encyclopaedia Britannica Online. 6 Nov 2009 <http://www.britannica.com/EBchecked/topic/230597/germ-layer>.
Marejeo zaidi
- Scott F. Gilbert. Developmental Biology. Sinauer, 2003. ISBN 0-87893-258-5.
- Lewis Wolpert. Principles of Development. Oxford University Press, 2006. ISBN 0-19-927536-X.
Viungo vya nje
- Chuo Kikuu cha Indiana Uhuishaji za Embriologia ya Binadamu Archived 16 Oktoba 2019 at the Wayback Machine.
- Kiinitete cha binadamu ndicho nini? Archived 25 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- UNSW Embriologia rasilimali kubwa ya maarifa na vyombo vya habari
- Ufafanuzi wa kiniitete kulingana na Webster Archived 30 Januari 2010 at the Wayback Machine.