Nenda kwa yaliyomo

Korentino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya kisasa.

Korentino (pia: Kaourintin, Corentin; 375 hivi - 12 Desemba 453) kadiri ya mapokeo, alikuwa askofu wa kwanza wa Quimper (Bretagne.

Habari zake zinapatikana katika Maisha ya Mtakatifu Korentino yaliyoandikwa miaka 1220-1235.

Baada ya kuwa mkaapweke huko Plomodiern, mfalme Gradlon aliamua kuanzisha jimbo huko Quimper akamteua Korentino awe askofu wa kwanza. Hivyo akamtuma Tours apewe daraja takatifu na Martino.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Desemba[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.