Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mwamba tumbawe

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maana ya matumbawe

[hariri chanzo]

"Matumbawe", "fufuwele" na "chawe" ni majina ya maada ya kabonati ya kalisi au chokaa inayounda miamba katika bahari. Chokaa hii hutolewa na wanyama wadogo ambao wanaunganishwa pamoja na kuunda makoloni makubwa. Wanyama hawa ni aina ya wanyama-upupu wa ngeli ya Anthozoa. ChriKo (majadiliano) 14:41, 9 Juni 2019 (UTC)[jibu]

Sawa ila kwa matumbawe naona pia matumizi kwa hali ya uhai, siyo mawe pekee yanayobaki. Lkn sijachungulia kwa undani.. ,Kipala (majadiliano) 16:51, 9 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Kweli? Uliona hii katika kamusi gani? Nilitafuta zaidi ya saa moja katika kamusi na kwenye internet, lakini sikupata mifano ya matumbawe kama viumbe hai. Ule karibu sana ulitumia "chechevule wa matumbawe". ChriKo (majadiliano) 18:21, 9 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Sijaona msaada wowote kwenye kamusi. Intaneti naona matumizi "miamba ya matumbawe= reef, matumbawe = corals", lakini nimechungulia kidogo tu, siwezi kusema kwa uhakika.
Mifano kadhaa: (google search: "kwenye matumbawe")
https://www.mzalendo.net/habari/makala-hali-ya-matumbawe-zanzibar.html
Kimsingi, mamilioni ya viumbe viishivyo baharini hutegemea matumbawe ili kuzaliwa na kukua vizuri na hatimae binadamu kunufaika navyo , samaki ambao ni chakula maarufu duniani kote, ni miongoni mwa viumbe hivyo. Inafahamika kuwa miamba ya matumbawe ni mojawapo ya vitu vya kuvutia katika maumbile ya dunia. ...... Hata hivyo, baadhi ya watu wanafikiri kuwa matumbawe ni aina ya mawe, lakini sio ukweli kwani huo ni mkusanyiko wa wanyama wadogo sana wanoitwa ‘polipu’ (polyps), ambao wana kiunzi cha mfupa mgumu kwa nje mithili ya jiwe. ... Polipu ambao wamehusiana na jejeta (mdudu wa bahari wa yavuyavu) na anemone, wana mikia yenye kuchoma wanayoitumia kwa kulia (plankitoni).
http://reefresilience.org/sw/management-strategies/managing-local-stressors/temporary-closures/
matumbawe yanaweza kuathirika zaidi ugonjwa na vyanzo vingine vya vifo. Katika baadhi ya matukio, kuzuia shughuli au kufunga maeneo ya miamba inaweza kuwa mkakati muhimu kwa wasimamizi ili kupunguza athari kwenye miamba ya maji wakati wa ongezeko la muda wa dhiki ya mazingira au wakati wa kupona.... Shughuli ambazo zinaweza kuwa lengo la jitihada za usimamizi wa ziada wakati wa matatizo makubwa ya matumbawe ni pamoja na:
  • Maji ya maji taka
  • Mawasiliano ya kimwili kutoka kwa aina mbalimbali au nanga
  • Uvuvi (hasa wa mifugo)
Kujua Wakati Wakorals Wanahitaji Msaada ..... Hatua ya kwanza katika kusaidia matumbawe kupitia vipindi vya shida ni kutambua wakati wao ni chini ya shinikizo.
http://reefresilience.org/sw/coral-reefs/stressors/local-stressors/coral-reefs-tourism-and-recreational-impacts/
Shughuli za burudani zinaweza kuharibu miamba ya matumbawe kupitia: Uvunjaji wa makoloni ya matumbawe na uharibifu wa tishu kutokana na mawasiliano ya moja kwa moja kama vile kutembea, kugusa, kupiga mateka, kusimama, au gear .... Kuvunjika au kuharibu makoloni ya matumbawe na uharibifu wa tishu kutoka nanga za mashua
www.dw.com/downloads/26374580/lbe-kis-environment-09-destructive-fishingps.pdf
(miamba ya matumbawe= reef, matumbawe = corals) Kipala (majadiliano) 20:06, 9 Juni 2019 (UTC)[jibu]