Studio za filamu, vituo vya televisheni, wasimulia hadithi, wachapishaji michezo na ligi za michezo hutumia Tenor ili kuwafikia watumiaji kwenye vifaa vya mkononi, kuongeza kutazamwa kwa GIF na kushiriki kunakochochea:
Kwa filamu ijayo ya Justice League, Warner Brothers walishirikiana na Tenor ili kuangazia GIF kutoka kwenye kionjo kinachosubiriwa kwa hamu. Ndani ya kipindi kisichozidi siku 5 baada ya kionjo kutolewa, maudhui ya GIF ya Tenor ya filamu ya Justice League yalitazamwa zaidi ya mara milioni 90 na kushirikiwa moja kwa moja mara mamia ya maelfu, kusababisha ongezeko kubwa la ushiriki ulipohitajika zaidi.
Changamoto ya Netflix ya mtiririko ni tofauti kabisa na televisheni ya mfululizo. GIF za vipindi vya Netflix huvuma katika wiki zinazokaribia kipindi cha utoaji, kwa hivyo Netflix imeshirikiana na Tenor ili kuendeleza kasi ya mawasiliano ya kijamii kwa kutumia GIF, na kuunda mtiririko endelevu wa vipindi vyake vya Narcos, Narcos, Master of None, {thecrownLink }, na filamu ijayo inayoangazia Will Smith, Bright.
Showtime imepata Maarifa muhimu kutoka Tenor kwa ajili ya kipindi chake kipya cha Billions na pia imefanikiwa hivi majuzi kushirikiana na Tenor katika kuibua upya maudhui ya Dexter kwa maadhimisho ya miaka 10 ya mfululizo huo. Mbali na kuangazia maudhui yanayovuma yanayotiririshwa, kutumia maudhui ya zamani na kukusanya mkakati wa GIF ambao hurejesha msisimko wa watumiaji ni lengo kuu la Timu ya Mafanikio ya Washirika wa Tenor.
Kwa kuhudumia zaidi ya watumiaji milioni 200 wanaoitumia kila mwezi na kuchakata zaidi ya maombi milioni 200 ya utafutaji ya kila siku, Tenor ndio mfumo mkubwa na unaokua kwa kasi zaidi wa kushiriki GIF kwenye vifaa vya mkononi. Programu yetu ya Kibodi ya GIF ndio aina inayopakuliwa zaidi kwenye iOS na Android. Na tunawezesha kushiriki GIF kwa washirika ikiwa ni pamoja na Apple iMessage, Facebook Messenger, WhatsApp, Google Gboard, Kik, LinkedIn, Touchpal na wengine.
{emotional GraphLink} inaambatisha hoja bilioni 4 tofauti za utafutaji kwenye GIF zinazoielezea vizuri zaidi. Ukiwa mshirika wa maudhui wa Tenor, tutajumuisha GIF zako kwenye mtambo huu thabiti wa kulinganisha na kuwasilisha maudhui yako katika matokeo ya utafutaji husika -- hatua inayowarahisishia watumiaji kuyapata, kuyashiriki na kuyafurahia.
Kama Mshirika wa Tenor utafaidika kupitia:
Timu ya Mafanikio ya Washirika wa Tenor itashirikiana nawe kwa karibu ili kuunda na kuratibu maudhui ya GIF ambayo yanafaa ili kufanikisha ushiriki wa watumiaji katika utumaji wa ujumbe kupitia kifaa cha mkononi. Tutajumuisha maudhui yako kwenye mfumo wetu na kuyaboresha ili yatumike kwenye vifaa vya mkononi. Grafu ya Hisia ya Tenor itaambatisha maudhui yako kulingana na hoja husika za utafutaji na kuyaonyesha wakati watumiaji wetu zaidi ya milioni 200 wanatafuta GIF mwafaka ili kuelezea mawazo na hisia zao kwa familia na marafiki.
Hatua ya kwanza: Tuzungumze! Wasiliana nasi sasa ili uanze kuchochea ushabiki kwa kushiriki GIF za kifaa cha mkononi.