Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

Bw. Gerald G. Mweli

Bw. Gerald G. Mweli
Katibu Mkuu

Prof. Peter L. M. Msoffe

Prof. Peter L. M. Msoffe
Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula)

Mha. Athumani J. Kilundumya

Mha. Athumani J. Kilundumya
Naibu Katibu Mkuu (Umwagiliaji na Zana za Kilimo)

Slide Photo
Wizara ya Kilimo na Taasisi zake zinashiriki katika “Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026”, kuonesha teknolojia mbalimbali kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma ambayo imeanza tarehe 16 hadi 23 Juni 2026, katika viwanja vya Chinangali chini ya kaulimbiu “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”,. Washiriki watapatiwa elimu kuhusu zoezi la upimaji wa Afya ya Udongo; Mazingira; Zana za kilimo; Masoko na Usalama wa Chakula; Sera pamoja na Mikakati ya Wizara ya Kilimo. Wizara inawalika wakulima na wadau kwa ujumla kutembelea banda la Wizara ya Kilimo na Taasisi zake ikiwemo, Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA); Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC); Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA); Bodi ya Sukari Tanzania (SBT); Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC); Bodi ya Pamba (TCB); Bodi ya Korosho pamoja na Bodi ya Kahawa.
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter L. M. Msoffe amewataka wakandarasi wanaotekeleza shughuli za ujenzi wa miradi Wilayani Rombo kukamilisha kwa wakati ili wananchi wanufaike na miradi ya Serikali. Naibu Katibu Mkuu Prof. Msoffe amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa soko la mazao eneo la Mamsera; ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Ushiri Ikuini; pamoja na ujenzi wa bwawa la umwagiliaji la Mrao Keryo tarehe 13 Juni 2026.
Slide Photo
Slide Photo
Slide Photo
Benki ya Kimataifa ya Japan inayoitwa Sumitomo Mitsui Banking Corporation (SMBC) imeonesha utayari wa kuwekeza katika Sekta ya Kilimo nchini kupitia uwezeshaji wa upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya ununuzi wa matrekta yatakayochangia kuongeza tija na kuimarisha uzalishaji wa kilimo. Akizungumza na ugeni kutoka nchini Japan tarehe 12 Juni 2026 jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, amesema mpango uliyowasilishwa na Benki hiyo unaendana na malengo ya Serikali ya kuwa na uwekezaji wa matrekta 10,000 hadi ifikapo mwaka 2030 hatua itayowawezesha wakulima kupata huduma ya zana za kısasa za kilimo kupitia vituo vya zana za kilimo nchi nzima.
Slide Photo
Slide Photo
Taasisi na Bodi za Wizara