Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
SIKU YA KIMATAIFA YA KUONDOA TAKA 2025 ILIVYOADHIMISHWA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA - DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi akisaini Mkataba wa makubaliano ya awali ya ukusanyaji taka za plastiki nchini kati ya NEMC na Kampuni ya GAIA CLIMATE ya Uturuki.
Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi akiongea na Waandishi wa Habari kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa kipindi cha Miaka minne.
Watumishi wa Baraza wakikabidhi majiko ya Nishati Safi ya kupikia (Gas stoves) kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Arusha tarehe 7/8/3025 siku moja kabla ya Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira-TAM (NEMC) Bi. Lilian Lukambuzi na kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt Immaculate Sware Semesi akiongea na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa jukwaa la usimamizi wa rasilimali za bahari lililofanyika katika hotel ya Johari Rotana Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ,Dkt.Immaculate Sware Semesi akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la usimamizi wa Rasilimali za bahari, uliofanyika katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchumi wa buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe.Zahor Kassim Mohamed (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi (kushoto kwake) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bi.Christina Mndeme (kulia kwake) pamoja na wajumbe wengine mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Usimamizi wa Rasilimali za Bahari katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa nchi wanachama zinazotekeleza Mradi wa kudhibiti matumizi ya kemikali ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu
Mradi wa kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu (AEHPMP), Mkutano wa nchi wanachama uliofanyika Tanzania katika Hotel ya Hyatt Regency October 4-12, 2024
Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP): Mkutano wa Nchi wanachama uliofanyika Tanzania katika Hoteli ya Hyatt Regency Oktoba 4-12,2024
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (NEMC) Bw. Dickson Mjinja (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Baraza pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kufungua mafunzo ya siku moja yahusuyo elimu ya Mazingira katika ukumbi wa Mikutano wa Baraza Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza na baadhi ya wajumbe wa Menejimeti kutoka Ofisi yake mara baada ya kuzuru Ofisi za NEMC Dar es Salaam kwa ajili ya kikao cha pamoja
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji (MB) atembelea banda la NEMC Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane 2024 katika viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe atembelea banda la NEMC Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane 2024 katika viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma.
Kikao cha wadau cha kujengeana uwezo wa kuboresha mifumo ya usimamizi wa taka ngumu kilichoandaliwa na NEMC-CSE. Kikao hicho kimefanyika katika hoteli ya New Africa iliyopo jijini Dar es Salaam
NEMC yampatia tuzo ya shukrani aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hifadhi Hai ya RUMAKI. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Meja Edward Gowele kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) (katika waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza mara baada ya kufanya kikao nao kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi Zanzibar Bw. Zahor Kassim Mohamed El Kharousy akitoa neno la ufunguzi kwenye Kikao cha Wadau kuhusu Usimamizi wa Bahari na rasilimali zake tarehe 8 Julai, 2024 katika Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam.
Elimu ya Mazingira yatolewa kwa washiriki wa maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Sabasaba
Watumishi wa NEMC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la NEMC Clinic ya biashara tayari kuwahudumia wananchi katika maonesho ya sabasaba
Msanii wa bongo fleva Bw. Mrisho Mpoto azuru banda la NEMC maonesho ya 48 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.
NEMC kupitia Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa dhahabu (EHPMP) yatoa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo kwenye Maonesho ya Wiki ya Madini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango ametembelea banda la NEMC kwenye maonesho ya Wiki ya Madini Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Philip Isdory Mpango(katikati) akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na Menejiment ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kuhutubia kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Cnter Dodoma.