Baaadhi ya Wadau wa Kemikali, wakifuatilia mada katika mafunzo ya Usimamizi na Matumizi Salama ya Kemikali kwa wadau wa Kemikali yaliyofanyika wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, Juni 11, 2026
Mtumishi wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Kati, Suitbert Sinduhije (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu madhara ya usimamizi na matumizi yasiyo salama ya Kemikali kwa wadau wa Kemikali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Hashork wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, Juni 11, 2026.
Mtumishi wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Kati, Fidelis Chrizant (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani katika mafunzo ya Usimamizi na Matumizi Salama ya Kemikali kwa wadau wa Kemikali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Hashork wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, Juni 11, 2026
Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (aliyesimama) akiwasilisha mada juu ya majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, katika mafunzo ya Usimamizi na Matumizi Salama ya Kemikali kwa wadau wa Kemikali yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hashork wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, Juni 11, 2026
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi na Matumizi Salama ya Kemikali kwa wadau wa Kemikali Mkoa wa Tabora (hawapo pichani) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hashork wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, Juni 11, 2026
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza wakati akifunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia (hawapo pichani), mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Arusha Corridor Spring Juni 5-6, 2026.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani), kufunga mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Arusha Corridor Spring Juni 5-6, 2026.
Baaadhi ya Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia, wakifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano Mkuu wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Arusha Corridor Spring Juni 5-6, 2026.
Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Eliamini Mkenga, akizungumza wakati akitoa neno la kuwaaga Watumishi wa Mamlaka katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Arusha Corridor Spring Juni 5-6, 2026.
Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Ziwa, John Wanjala akizungumza na wasimamizi wa kemikali kutoka Kanda ya Ziwa (hawapo pichani), wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wasimamizi hao yaliyofanyika kuanzia Mei 19 hadi 20, 2026, mkoani Mwanza.