Nenda kwa yaliyomo

Fundo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 21:47, 11 Mei 2021 na Kipala (majadiliano | michango) (Created by translating the page "Knot")
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Fundo kati ya kamba buluu na nyekundu


Fundo ni namna ya kuunganisha pande mbili za kamba, uzi au kitambaa, dutu kinamo kama mpira au wakati mwingine pia za nyororo.

Namna ya kupinda pande mbili kati yao inaongeza uso zinapogusana na hivyo kuongeza msuguano wakati pande mbili zinavutwa; msuguano huo unazuia kuteleza kwa kamba juu ya kamba. Kila fundo inapokazwa huwa imara zaidi.

Mafundo yamepatikana tangu kale, wakati binadamu walianza kutumia vikonyo vya mimea au nyuzi nyingine kufunga mawe kwenye pini za shoka zao. Mafundo yalitumiwa pia kwa kutengeneza nyavu au matego.

Mafundo yaliendelea sana kuwa tata tangu kupatikana kwa mashua ya tanga.

Kati ya mabaharia elimu ya mafundo imekuwa sayansi ya pekee. Waljifunza na kufundishana kutumia mafundo mbalimbali ka shughuli maalumu.