Valentinus
Valentinus (Terni, Italia, 176 hivi - Roma, 14 Februari 273) ni jina la Mkristo mfiadini , padri au askofu wa Terni, ambaye anaheshimiwa kama mtakatifu katika Kanisa Katoliki, lakini pia na Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri kadhaa.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Februari ya kila mwaka (Valentine's Day).
Historia
Historia yake inawezekana inamchanganya na Valentinus mwingine, padri wa karne ya 3 huko Roma, aliyeuawa mwaka 269 katika mazingira yaleyale.
Hadithi
Kuna hadithi mbalimbali juu yake.
Hadithi mojawapo inasema Valentinus aliandika barua kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.
Toka hapo Valentinus anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani.
Marejeo
- The Golden Legend: St. Valentine
- Catholic Encyclopedia: St. Valentine
- Diocese of Terni. 2009. Saint Valentine
- In Search of St. Valentine
- Oruch, Jack B. 1981. "St. Valentine, Chaucer, and Spring in February", Speculum 56.3 (July 1981), pp 534–565.
- Paglia, Vincenzo. 2007. "Saint Valentine's Message".Washington Post, February 15, 2007.