Nenda kwa yaliyomo

Wakamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 11:50, 18 Februari 2019 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Kazi ya Kikamba katika duka la Mombasa.

Wakamba ni kabila la watu wa Kenya wakikalia eneo la Ukambani kati ya Nairobi, Voi na kati ya mlima Kenya na mlima Kilimanjaro. Wakamba ni kabila kubwa la nne nchini Kenya.

Hutumia lugha ya Kikamba ambacho ni lugha ya Kibantu karibu na Kigikuyu, Kiembu na Kimeru.

Maisha kabla ya ukoloni

[hariri | hariri chanzo]

Asili yao inaaminika kuwa katika eneo la Kilimanjaro yenyewe lakini walihama takriban miaka 400-500 iliyopita kuja Ukambani walipo. Walikuwa wafugaji, wakulima na wawindaji.

Katika karne ya 19 walikuwa na nafasi muhimu katika biashara ya pembe za ndovu kati ya bara na pwani ya Kenya. Misafara yote kutoka au kwenda Mombasa ilipaswa kupita katika eneo lao. Walitafutwa sana kama wapagazi.

Maisha wakati wa ukoloni

[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia miaka ya 1930 Wakamba walianza kujiunga kwa wingi na jeshi na polisi ya kikoloni. Imekadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya Wakamba wote walioajiriwa walikuwa jeshini. Mwendo huo ulisababishwa na ugumu wa maisha kutokana na ukame wa Ukambani kwa upande mmoja na hali ya kukaa karibu na reli na taasisi za dola la kikoloni kwa upande mwingine.

Wakati wa vita vya Mau Mau sehemu za Wakamba walijiunga na harakati ile, lakini wanajeshi kwa ujumla walisimama upande wa serikali ya kikoloni.

Katika kilimo Wakamba walianza kilimo cha umwagiliaji.

Wasanii Wakamba wamekuwa maarufu kama wachongaji wa ubao nchini Kenya. Katika historia yao hutunza kumbukumbu ya kwamba wakati wa ukoloni Mkamba alifika Dar es Salaam alipojifunza sanaa hiyo kutoka kwa wachongaji Wamakonde na kurudi na maarifa aliyofundisha wengine. Leo hii ni hasa Wakamba wanaochonga sanamu za wanyamapori zinazotafutwa na kununuliwa na watalii.

Wakamba maarufu

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakamba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.