Bunzi (Eumeninae)
Bunzi | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bunzi mweusi (Anterhynchium fallax)
“Mitungi” ya matope ya bunzi
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Jenasi ±200, spishi ±3000; jenasi 32 katika Afrika ya Mashariki:
|
Bunzi ni nyigu wa nusufamilia Eumeninae katika familia Vespidae. Spishi nyingi zina kiuno chembemba sana na mara nyingi kirefu (petiole), lakini kiuno cha spishi nyingine ni kifupi na si chembamba sana. Bunzi wanaojulikana sana hutengeneza vijengo kwa matope vilivyo umbo la mtungi mdogo.
Nusufamilia hii ni kubwa kuliko zote za Vespidae yenye takriban jenasi 200 na karibu na spishi 3000.
Nyigu wa familia Sphecidae huitwa bunzi pia. Halafu kuna bunzi-buibui wa familia Pompilidae.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Bunzi wa Eumeninae ni baini ya nyigu wanaojulikana sana katika Afrika ya Mashariki. Spishi zinazoonekana sana ni nyeuzi na mara nyingi zina mng'ao buluu, urujuani au kijani. Spishi nyingine zina miviringo, mistari au madoa njano, meupe, machungwa au mekundu au miungano ya rangi hizo.
Kuna spishi zenye kiuno chembamba na kirefu, na spishi nyingine zenye kiuno kifupi kisicho chembamba sana. Urefu wao ni chini ya sm 1 hadi takriban sm 5.
Mwenendo
[hariri | hariri chanzo]Bunzi hutaga mayai yao katika vyumba vya matope. Vyumba hivyo vinaweza kujengwa nje kimoja-kimoja au katika vikundi vya vyumba kadhaa kwenye miamba au miti au hata kwenye kuta au milango ya nyumba. Vijengo vya chumba kimoja vina umbo la mtungi kwa kawaida. Vile vilivyo vyumba kadhaa havina umbo maalum. Bunzi wanaweza kujenga vyumba pia katika vishimo walivyochimba wao wenyewe au katika vishimo vya wadudu wengine vilivyoachwa au hata katika matundu yaliyofanywa na watu, kama matundu ya misumari au ya funguo au katika vifaa vya elektroniki.
Kabla ya kutaga jike hukamata viwavi, mabuu ya mbawakawa au buibui. Anadunga wadudu hao na kuingiza sumu ili kuwapoozesha. Anaweka mmoja au wawili katika chumba kimoja. Kisha anataga yai moja juu ya mdudu au analining'inia kutoka dari. Buu akitoka katika yai huanza kujilisha kwa mdudu aliye bado ni hai na mbichi.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Vikundi vya vyumba
-
Vyumba katika ukuta
-
Delta emarginatum
-
Eumenes mediterraneus