Eskişehir
Eskişehir (eskē'shehēr, Kituruki: Eskişehir, "Mji wa Kale"; Kilatini Dorylaeum; Kigiriki: Δορύλαιον, Dorylaeum) ni jiji lililopo kaskazini-magharibi mwa ya Uturuki na ndiyo mji mkuu wa Jimbo la Eskişehir.
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2008, idadi ya watu wanaoishi katika mji imekadiriwa kufikia kiasi cha 614,247 ambao 599,796 wanaishi katikati ya jiji la Eskişehir.[1] Jiji lipo katika ukingo wa Mto Porsuk, takriban mita 792 kutoka juu ya usawa wa bahari, ambamo inatizama mapolomoko ya Phrygia.
Katika vilima vya karibu kuna visima vya maji ya moto. Takriban km 250 kutoka jiji hapa kuelekea mjini magharibi mwa Ankara, na km 350 kusini-mashariki ya jiji la Istanbul pia km 90 kutoka jiji hapa na kuelekea kaskazini-mashariki mwa mji wa Kütahya. Mji huu una eneo la kilomita za mraba zipatazo 2,678.[2]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Jina la mji la Eskişehir linamaa ya Mji wa Kale kwa lugha ya Kituruki, ingawa neno la kwanza la şehir linatokana na Kiajemi yaani neno shahr (Kiajemi: شهر), ina maana ya "mji". Mji hasa ulianzishwa na Waphrygia mnamo mwaka wa 1000 KK. Vinyago na masananmu mengi ya Waphrygia bado yanapatikana katika Majumba ya Sanaa ya Mambo ya Kale.
Pia kuna majumba ya maonyesho ya mawe ya meerschaum, ambazo shuhuli zake bado zinatamba hadi leo, ambavyo leo hii vinatumika kutengenezea kiko za kuvutia tumbaku zenye ubora hali ya juu. Mnamo karne ya nne AD, karibuni km 10 zilisogea kaskazini-mashariki mwa Karadja Hissar hadi Shehir Euyuk.
Muda wowote mji ukiwa unatajwa na wanajigrafia wa kale, basi walikuwa wakiuelezea kama moja kati ya miji mizuri ya Anatolia.
Kama jinsi ilivyo miji mingi ya Anatolia, Ukristo ulifikia baada ya Konstantine Mkuu aliyefanya kama dini rasmi ya Dola la Rom. Kuanzia karne ya nne, rekodi zilizopo zinaonyesha kwamba maaskofu wameanza kumiliki maofisi yao mjini Eski؛ehir. Hapo zamani mji ulikuwa ukijulikana kama Dorylaeum. Miongoni mwa maaskofu hawa, alikuwepo Eusebius, alikuwa akihusika sana na kuendeleza siri na itikadi ya kanisa.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Vivutio
[hariri | hariri chanzo]Elimu
[hariri | hariri chanzo]Utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Eski؛ehir ni mji mkavu na wenye baridi, theuluji na joto, kiangazi. Mvua mara nyingi hutokea wakati bubujiko na kipupwe.
Months | Jan | Feb | Mar | Apr | Mei | Jun | Jul | Ago | Sep | Oct | Nov | Dec |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Avr.Max. °C | 3.9 | 6.2 | 11.2 | 16.4 | 21.8 | 25.9 | 29.2 | 28.9 | 25 | 19.8 | 12.4 | 5.5 |
Avr.Min °C | -4.1 | -3.9 | -1.5 | 2.8 | 6.9 | 10.4 | 13.1 | 13 | 8.4 | 4.4 | 0.3 | -2 |
Michezo
[hariri | hariri chanzo]Klabu | Michezo | Imeazishwa | Ligi | Uwanja |
---|---|---|---|---|
Eski؛ehirspor | Mpira wa Miguu | 1965 | Turkcell Super League (Turkish Premier Division) | Eski؛ehir Atatürk Stadium |
Anadolu University | Mpira wa Kikapu | ? | Turkish Basketball League 2 | Anadolu University Sports Hall |
Watu mashuhuri
[hariri | hariri chanzo]- Battal Gazi - mtakatifu mwislamu aliyezikwa Seyitgazi
- Yunus Emre - karne ya 13 mshairi asilia wa Kituruki
- Sheik Edebali - karne ya 13 kiongozi wa kidini, mwanzilishi wa dini ya Dola la Osmani
- Behiç Erkin - Mturuki Schindler aliyezaliwa mjini İstanbul, alizalikwa katika kituo cha treni cha mjini Eski؛ehir
- Cüneyt Arkın - Nyota wa Filamu
- Serpil اakmaklı - Nyota wa Filamu
- Yılmaz Büyüker؛en - Meya wa Eski؛ehir
- Zeki Sezer - Kiongozi wa DSP
- İlhan Mansız - Mchezaji mpira wa miguu
- Neslihan Demir Darnel - Mchezajiwa Volleyball
- Ersan Ilyasova - Mchezaji wa mpira wa kikapu
- Kerem Gِnlüm - Mchezaji wa mpira wa kikapu
- Azra AKIN - Mrembo wa Dunia
- Ertugrul Algan PhD.- Mhadhiri, Mpiga picha, Mtunzi wa vitabu
Picha za mji huu
[hariri | hariri chanzo]-
Museum of glassware arts -
Old houses in Odunpazarı -
Mothers' Memorial -
A view from downtown
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ TC Eskişehir Valiliği – Nüfus Durumu Archived 28 Februari 2009 at the Wayback Machine. (Kituruki)
- ↑ Statoids. "Statistical information on districts of Turkey" (kwa English). Iliwekwa mnamo 2008-04-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)
Malezo zaidi
[hariri | hariri chanzo]- Falling Rain Genomics, Inc. "Geographical information on Eski؛ehir, Turkey" (kwa English). Iliwekwa mnamo 2008-04-03.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - Municipality of Eski؛ehir, Turkey. "General information on Eski؛ehir" (kwa English). Iliwekwa mnamo 2008-04-03.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) Eskişehir travel guide kutoka Wikisafiri
- (Kituruki) District governor's official website
- Map of Eski؛ehir central district Archived 3 Machi 2009 at the Wayback Machine.
- (Kituruki) District municipality's official website
- (Kituruki) Eski؛ehir Police Headquarters
- (Kituruki) Local information website
- (Kituruki) Local information website with Panaromic Photos Archived 11 Mei 2020 at the Wayback Machine.
- (Kituruki) Eskişehir Photo Gallery
- (Kituruki) http://www.ertugrulalgan.net Archived 8 Januari 2010 at the Wayback Machine.