Nenda kwa yaliyomo

Kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kaya (kwa Kiingereza household) ni kundi la watu wanaoishi mahali pamoja kama familia. Kwa maana nyingine ni nyumba wanapoishi.

Istilahi hiyo inayotumiwa katika takwimu za watu, kwa mfano wakati wa sensa. Ufafanuzi wa kawaida ni "watu wanaokaa pamoja na kula pamoja". Mjini kaya inaweza kukaa katika chumba kimoja. Mashambani inawezekana kuna familia inayokalia kwa pamoja vyumba kadhaa vya jirani. Kwa maana ya takwimu kaya inaweza kuwa hata mtu mmoja tu akiishi peke yake.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kwa asili kaya ilikuwa eneo la nyumba moja au nyumba jirani ambako ukoo mmoja ulikaa.

Charles Sacleux (1939) alieleza kuwa wakati wake kwa watu wa nyika "Kaya" ilikuwa kijiji kikuu, mara nyingi kijiji anapokaa chifu, mara nyingi pia kijiji kilichoimarishwa kwa fensi au ukuta[1].

Ludwig Krapf (1882) aliandika: "The chief place, the residence, meeting place of the Wanika; usually fortified in case of sudden war"[2]

  1. www.uni-leipzig.de/~afrika/swafo/documents/Sacleux1939_small_size_290_MB.pdf Kamusi ya Sacleux kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Leipzig], uk. 337
  2. Krapf, Ludwig: A dictionary of the Suahili language, London 1882, uk. 133
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kaya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.