Kietruski
Mandhari
Kietruski ni lugha ya Waetruski wa kale waliokali sehemu za katikati za Italia wakati wa milenia ya 1 KK.
Lugha yenyewe ilipotea katika karne ya 1 BK na Waetruski wa mwisho walihamia kwa matumizi ya Kilatini na Kigiriki. Lakini kuna mabaki mengi ya utamaduni wao yaliyohifadhiwa hasa ukutani wa makaburi lakii pia kwa njia ya mifano michache ya maandishi usoni wa bati au kitambaa.
Vitabu yva Waroma wa kale vimehifadhi kumbukumbu kuhusu vitabu vingi vya Waetruski lakini hivi vyenyewe haviko tena. Waakiolojia hukusanya mabaki yao wakijaribu kuyaelewa na kuyaeleza.
Mwandiko wa Kietruski ulikuwa na msingi aktika alfabeti ya Kigiriki na mwandiko wa Wafinsia.