Nenda kwa yaliyomo

Kroatia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Republika Hrvatska
Jamhuri ya Kroatia
Bendera ya Kroatia Nembo ya Kroatia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Kihistoria: Antemurale Christianitatis (Kilatini)
"Ngome ya Ukristo"
Wimbo wa taifa: "Lijepa naša domovino"
"Nchi yetu nzuri"
Lokeshen ya Kroatia
Mji mkuu Zagreb
45°48′ N 16°0′ E
Mji mkubwa nchini Zagreb
Lugha rasmi Kikroatia1
Serikali Jamhuri
Zoran Milanović
Andrej Plenković
Uhuru
Ilianzishwa
Utemi wa Kroatia
Ufalme wa Kroatia
Kutoka Yugoslavia

Karne ya 7 (mwanzoni)
3 Machi 852
925
25 Juni 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
56,542 km² (ya 126)
0.01
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
4,551,000 (ya 128)
4,284,889
75.8/km² (ya 126)
Fedha Kuna (kn)  (HRK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .hr
Kodi ya simu +385

-

1pia Kitalia katika Istria.



Ramani ya Kroatia
Uwanja wa Arena (colosseum) mjini Pula, Istria

Kroatia (pia Korasia, kwa Kikroatia: Republika Hrvatska) ni nchi ya Ulaya ya kusini-mashariki. Imepakana na Slovenia, Hungaria, Serbia, Bosnia na Herzegovina na Montenegro.

Ng'ambo ya kidaka cha Adria iko Italia.

Mji mkuu ni Zagreb.

Kroatia ilikuwa kati ya majimbo ya Yugoslavia na ilipata uhuru wake mwaka 1991.

Imejiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Julai 2013.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo ya Kroatia yalikuwa sehemu ya Illyria wakati wa Dola la Roma na kutawaliwa kama mikoa ya dola hilo.

Mnamo mwaka 395 Dola la Roma liligawiwa katika sehemu ya magharibi na sehemu ya mashariki. Sehemu hizo mbili ziliendela baadaye kwa namna mbili tofauti.

Kuanzia mwaka 600 makabila ya Waslavoni walianza kuingia na kukaa. Wakroatia waliunda utemi wao wa kwanza. Kroatia ilikuwa upande wa magharibi wa mstari wa mwaka 395, hivyo chini ya athira ya Kanisa Katoliki, ikaendelea kuwa sehemu ya utamaduni wa Ulaya ya magharibi. Kumbe Waslavoni wa jirani wanaotumia lugha ileile waliishi chini ya athira ya Bizanti na Kanisa la Kiorthodoksi, hivyo kuendelea kama sehemu ya Ulaya ya Mashariki na kuitwa Waserbia.

Mtemi Tomislav (910928) alichukua cheo cha mfalme mwaka 925. Huo Ufalme wa Kroatia uliendelea hadi mwaka 1102. Wakati ule mfalme wa mwisho hakuwa tena wa watoto na mfalme wa Hungaria alichaguliwa kuwa mfalme wa Kroatia pia. Maungano hayo na Hungaria yaliendelea kwa karne nyingi.

Tangu maungano wa Hungaria na Austria ni Kaisari wa Austria aliyekuwa na cheo cha mfalme wa Krotia hadi vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918).

Mwaka 1918 Dola la Austria liliporomoka. Waslavoni wa Kusini waliamua kuunda ufalme wa pamoja kwa jina la Yugoslavia. Kroatia ilikuwa sehemu ya Yugoslavia kuanzia 1918; kwanza katika ufalme wa Yugoslavia, halafu katika jamhuri ya kisoshalisti ya Yugoslavia hadi 1991.

Miaka 1990 / 1991 Yugoslavia iliporomoka na majimbo yake zilitafuta uhuru kama nchi za kujitegemea.

Nchi ina umoja mkubwa upande wa kabila, lugha na dini, watu wengi wakiwa Wakroatia asilia (90.4%), wakisema Kikroatia (95.6%) na kufuata imani ya Ukristo katika Kanisa Katoliki (86.28%).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kroatia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.