Kurene
Kurene (kwa Kigiriki Κυρήνη, Kyrēnē) ulikuwa mji wa Libya mashariki uliofuata ustaarabu wa Ugiriki wa kale halafu Roma ya kale. Uko karibu na Shahhat ya leo.
Ulikuwa wa kale na muhimu kuliko miji mitano ya Kigiriki ya mkoa ambao kutokana na jina lake unaitwa hadi leo Cyrenaica.
Mwaka 1982 ulitangazwa na UNESCO kuwa kituo cha Urithi wa Dunia.[1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ulianzishwa na Wagiriki mwaka 630 KK
Uliitwa pengine "Athens ya Afrika", pia kutokana na shule ya falsafa iliyoanzishwa huko.[2][3][4]
Katika karne ya 4 BK mji ulibaki mahame.
Katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Kurene unatajwa katika kitabu cha pili cha Wamakabayo, kimojawapo cha vitabu vya Deuterokanoni, kama mji wa asili wa Jasone wa Kurene, Myahudi wa Kigiriki aliyeandika mfululizo wa magombo 5 juu ya Historia ya Wamakabayo. Mtunzi wa 2Mak alikiri kuwa amefupisha tu magombo hayo.
Kurene unatajwa hasa katika Agano Jipya. Injili ndugu zinamtaja Myahudi mwingine wa mji huo, Simoni wa Kurene, baba wa Aleksanda na Rufo (Mk 15:21 na madondoo sambamba), kuwa ndiye aliyemsaidia Yesu kubeba msalaba hadi Kalivari.
Matendo ya Mitume 2:10 kinasimulia kwamba Wayahudi kutoka Kurene walikuwa kati ya watu ambao siku ya Pentekoste ya mwaka wa kifo cha Yesu huko Yerusalemu waliwasikia Mtume Petro na wenzake kuhubiri ufufuko wa Yesu na ubatizo.
Tena Mdo. 6:9 kinasimulia kuwa Wayahudi kutoka mji huohuo walikuwa kati ya wale walioshindana na Stefano na hatimaye wakamuua kwa usimamizi wa atakayekuwa Mtume Paulo.
Halafu Mdo. 11:20 kinasema kuwa Wakristo wenye asili ya Kurene (pamoja na wenzao kutoka Kupro) walikuwa wa kwanza kuwahubiria wasio Wayahudi.
Hatimaye Mdo. 13:1 kinamtajia Lukio wa Kurene kati ya viongozi wa Kanisa huko Antiokia.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "21 World Heritage Sites you have probably never heard of". Daily Telegraph.
- ↑ Temehu (Cyrene)
- ↑ Global Treasures: Cyrene
- ↑ "للغة العربية اضغط هنا http://cyreen630.maktoobblog.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-23. Iliwekwa mnamo 2015-10-08.
{{cite web}}
: External link in
(help)|title=
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Cyrene project summary Archived 9 Desemba 2010 at the Wayback Machine. at Global Heritage Fund
- Explore Cyrene with Google Earth Archived 17 Agosti 2011 at the Wayback Machine. on Global Heritage Network
- Cyrene and the Cyrenaica Archived 31 Desemba 2008 at the Wayback Machine. by Jona Lendering
- University of Pennsylvania Museum excavations at Cyrene
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kurene kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |