Jamhuri ya Roma
Mandhari
Jamhuri ya Roma ilikuwa kipindi cha Roma ya Kale ambako mji na milki yake ilitawaliwa kwa mfumo wa jamhuri.
Kipindi hiki kilianzia baada ya kufukuzwa kwa mfalme wa mwisho mwaka 509 KK na kwisha katika mabadiliko ya serikali wakati wa Caesar na Augusto.
Wakati wa jamhuri Waroma walifuata mfumo ufuatao:
- Mtu aliweza kushika cheo chochote kwa muda wa mwaka moja pekee
- Kama ameshika cheo fulani alikataliwa kuwa na kipindi cha pili.
- Vyeo vyote serikalini vilishikwa na watu wawili waliopaswa kukubaliana; kila mmoja alikuwa na haki ya kufuta maazimio ya mwenzake.
- Wanasiasa walipaswa kufuata utaratibu wa kugombea vyeo serikalini katika ufuatano
- Kama mtu ameshika cheo alipaswa kupumzika miaka miwili kabla ya kugombea cheo kilichofuata.
Cheo kimoja cha dikteta pekee kilishikwa na mtu mmoja lakini muda wake kilibanwa kuwa miezi sita tu.
Mfumo huu ulilenga kuzuia kurudi kwa wafalme au kumpa mtu yeyote madaraka yaliyolingana na mfalme.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Roma kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |