Mkunga (samaki)
Mkunga | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkunga-chui mkubwa (Gymnothorax javanicus)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 8: |
Mikunga ni samaki wa baharini na/au maji baridi katika oda Anguilliformes walio na umbo la nyoka.
Hufanyiwa maendeleo makubwa kutoka hatua ya mapema ya lava hadi hatua ya mwisho ya waliokomaa, na wengi ni samaki mbuai.
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]Mikunga ni samaki waliorefuka wenye urefu wa sm 5 katika Mkunga Taya-moja (Monognathus ahlstromi) hadi m 4 katika Mkunga-chui Mkubwa Mwembamba. Waliokomaa wana uzito kutoka g 30 hadi zaidi ya kg 25.
Hawana mapezi ya tumbo, na spishi nyingi hazina mapezi ya mbavu pia. Mapezi ya mgongo na ya mkundu yameungana na pezi la mkia na pamoja yanaunda utepe mmoja unaoenda kiasi cha urefu wa mnyama. Mikunga huogelea kwa kuzalisha mawimbi ya mwili ambayo husafiri urefu wa mwili wao. Wanaweza kuogelea kisengesenge kwa njia ya kupindua mwelekeo wa wimbi.
Mikunga wengi sana huishi katika maji kame ya bahari na huingia kwenye mchanga, matope au katikati ya miamba. Takriban spishi zote za mikunga hukiakia usiku na kwa hivyo huonekana kwa nadra. Wakati mwingine huonekana wakiishi pamoja katika mashimo yaitwayo "mashimo ya mikunga". Spishi fulani za mikunga huishi katika maji ya kina kirefu zaidi ya matako ya mabara na ya miteremko yao yenye kina cha hadi m 4,000. Wanajenasi wa Anguilla hukaa maji baridi kwa muda mrefu, lakini hata hawa wanarudi baharini ili kuzaliana.
Mzunguko wa maisha
[hariri | hariri chanzo]Mikunga huanza maisha yao kama lava angavu inayoitwa leptocephali. Lava wa mikunga huelea kwenye maji yaliyo juu ya bahari, wakijilisha theluji ya bahari, chembe ndogo zinazoelea ndani ya maji. Halafu hubadilika umbo kuwa mikunga-kioo na kisha kuwa mikunga wachanga kabla ya hatimaye kutafuta makazi yao ya kitoto na yale ya waliokomaa. Mikunga wengi wanabakia baharini muda wa maisha yao yote, lakini mikunga wachanga wa maji baridi wa familia Anguillidae husafiri katika mito dhidi ya mkondo na wanalazimika kupanda juu ya vikwazo kama vile vizingiti, kuta za maboma ya maji na maporomoko ya maji ya asili.
-
Mayai ya mikunga yanatoa lava wa hatua leptocephalus...
-
...na wanakuwa mikunga-kioo wakiingia maji baridi kutoka bahari
-
Wanaogelea dhidi ya mkondo kama mikunga wachanga wa maji baridi
-
Mikunga-fedha waliokomaa huhama kurudi bahari
Mwainisho
[hariri | hariri chanzo]Mwainisho huu unafuatia "FishBase" ukigawanya mikunga katika familia 20. Familia za ziada zilizojumuishwa katika miainisho mingine (hasa ITIS na Systema Naturae 2000 zinajulikana chini ya familia iliyo ni kisawe chake katika mfumo wa FishBase.
Kutambua jadi ya spishi za maji baridi ilikuwa tatizo. Uchunguzi wa kijenomu unaonyesha kuwa ni kundi la nasaba moja lililotoka baina ya mikunga wa bahari.
- Nusuoda: Protanguilloidei
- Familia: Protanguillidae
- Nusuoda: Synaphobranchoidei
- Familia: Synaphobranchidae (inajumuisha Dysommidae, Nettodaridae na Simenchelyidae)
- Nusuoda: Muraenoidei
- Familia: Heterenchelyidae
- Familia: Myrocongridae
- Familia: Muraenidae
- Nusuoda: Chlopsoidei
- Familia: Chlopsidae
- Nusuoda: Congroidei
- Familia: Congridae (inajumuisha Macrocephenchelyidae na Colocongridae)
- Familia: Derichthyidae (inajumuisha Nessorhamphidae)
- Familia: Muraenesocidae
- Familia: Nettastomatidae
- Familia: Ophichthidae
- Nusuoda: Moringuoidei
- Familia: Moringuidae
- Nusuoda: Saccopharyngoidei
- Familia: Eurypharyngidae
- Familia: Cyematidae
- Familia: Monognathidae
- Familia: Saccopharyngidae
- Nusuoda: Anguilloidei
- Familia: Anguillidae
- Familia: Nemichthyidae
- Familia: Serrivomeridae
Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Anarchias seychellensis, Mkunga-chui wa Shelisheli (Seychelles moray)
- Anguilla labiata, Mkunga Mgongo-madoa (African mottled eel)
- Brachysomophis crocodilinus, Mkunga-nyoka Mamba (Crocodile snake eel)
- Chlopsis dentatus, Mkunga-chui Bandia Madoadoa (Mottled false moray)
- Conger cinereus, Mkunga-samaki au Mkunga Kijivu wa Afrika (Longfin African conger)
- Echidna leucotaenia, Mkunga-chui Uso-mweupe (Whiteface moray)
- Gymnomuraena zebra, Mkunga-chui Punda-milia (Zebra moray)
- Gymnothorax javanicus, Mkunga-chui Mkubwa (Giant moray)
- Gymnothorax margaritophorus, Mkunga-chui Shingo-mabaka (Blotch-necked moray eel)
- Monopenchelys acuta, Mkunga-chui Uso-mwekundu (Redface moray)
- Muraenesox bagio, Kowe au Koe (Common pike conger)
- Pseudechidna brummeri, Mkunga-chui Utepe Mweupe (White ribbon eel)
- Rhinomuraena quaesita, Mkunga-chui Utepe Buluu (Ribbon eel)
- Scuticaria tigrina, Mkunga-chui Madoadoa (Tiger reef eel)
- Synaphobranchus brevidorsalis, Mkunga-kookatwa Pezimgongo-fupi ( Shortdorsal cutthroat eel)
- Uropterygius polyspilus, Mkunga-chui Madoa-makubwa (Large-spotted snake moray)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mkunga wa Bengali
-
Mkunga-nyoka mamba
-
Mkunga-chui bandia rangi-mbili
-
Mkunga-samaki
-
Mkunga-chui nyota
-
Mkunga-chui punda-milia
-
Mkunga-chui shingo-mabaka
-
Mkunga-chui uso-mwekundu
-
Kowe kijivu
-
Mkunga-chui utepe mweupe
-
Mkunga-chui utepe buluu
-
Mkunga-chui madoadoa
-
Mkunga-kookatwa pezimgongo-fupi
-
Mkunga-chui kijani
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Mikunga kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 21 Desemba 2017 kwenye Wayback Machine.