Historia ya Malta
Historia ya Malta inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Malta.
Malta ilikaliwa na watu tangu milenia ya 4 KK. Kuna maghofu ya hekalu la mwaka 3200 KK hivi.
Baadaye funguvisiwa lilitawaliwa na Wafinisia, Karthago na Dola la Roma.
Malta inatajwa katika Biblia kwa sababu Mtume Paulo aliponea huko baada ya kuzama kwa merikebu alimosafiri baharini kuelekea Roma (Mdo 27:39 n.k.).
Waarabu walivamia visiwa hivyo mwaka 870 na kuvitawala hadi 1091.
Baadaye vilitawaliwa na Wanormandi wa Italia Kusini, baadaye tena na Wahispania chini ya mamlaka ya Dola Takatifu la Kiroma la Ujerumani.
Tangu mwaka 1530 visiwa vilikabidhiwa na Kaisari kwa askari wa Vita vya msalaba wa Chama cha Wanahospitali wa Mt. Yohane wa Yerusalemu.
Wanamisalaba hao walikuwa mabwana wa visiwa hadi Napoleoni alipoteka Malta mwaka 1799 akiwa safarini kwenda Misri.
Uingereza ulitwaa visiwa kutoka kwa Ufaransa ukatawala Malta hadi uhuru wake tarehe 21 Septemba 1964.
Tarehe 13 Desemba 1974 Malta ikatangazwa kuwa jamhuri ndani ya Jumuiya ya Madola.
Tarehe 1 Mei 2004 nchi ikajiunga na Umoja wa Ulaya.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Malta kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |