Mti Quotes

Quotes tagged as "mti" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Murphy. Sina mbinu zozote za kujikinga kama unavyojua; mbali na mafunzo ya FBI. Baada ya kumrusha nyoka wa Lisa nywele zilinisisimka. Wazo la kukimbia likaja ghafla. Kukimbia hata hivyo nikashindwa kwa kuhofu huenda wangeniona. Hivyo, nikarudi nyuma ya nyumba na kupanda mti na kujificha huko. Bunduki zilipolia, nilijua wamekuua. Ila kitu kimoja kikanishangaza: mashambulizi hayakuonekana kukoma. Kitu hicho kikanipa nguvu kwamba huenda hujafa na ulikuwa ukipambana nao. Kimya kilipotokea nilijua umewashinda nguvu, kitu ambacho kumbe kilikuwa kweli. Nilipokutafuta baadaye lakini bila kukuona kutokana na kukurukakara za maadui niliamua kwenda katika gari ili nije na gari kama mgeni, nikitegemea waniruhusu kuingia ili nipate hakika kama wamekuua au bado uko hai. Wasingenifanya chochote. Kimaajabu, niliposhuka katika mti ili nikimbie katika gari, niliona gari ikija kwa kasi. Kuangalia vizuri nikakuta ni Ferrari, halafu nikashangaa nani anaendesha gari ya Lisa!”
Murphy alitabasamu tena na kuendelea kusikiliza.
“Sijui moyo wangu ulikuwaje. Sikuogopa tena! Badala yake nilikaza mwendo na kuendelea kuifuata huku nikipata wazo hapohapo kwamba mtu aliyekuwemo akiendesha hakuwa adui. Adui angeingia katika gari na kunisubiri aniteke nyara.” Debbie alitulia.
“Ulihisi ni mimi?” Murphy aliuliza.
“Nilihisi ni mtu tu mwema amekuja kunisaidia ... au mwizi wa gari. Hata hivyo, baadaye nilijua ni wewe na furaha yangu yote ilirudi.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho – Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu – Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa – walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.”
Enock Maregesi