Wasiwasi Quotes

Quotes tagged as "wasiwasi" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Murphy hakupenda kupoteza muda. Alinyanyuka na kumimina risasi, Mungu akamsaidia akadondosha wawili huku wengine wakipotea kwa kuruka vibaya na kukwepa. Kwa kasi Murphy alikimbia huku ameinama mpaka katika milango mikubwa ya nje, ambayo sasa ilikuwa wazi. Hapo akasita. Chochote kingeweza kumpata kwa nje kama hangekuwa mwangalifu. Bunduki yake ilishakwisha risasi. Aliitupa na kuchungulia nje akaona adui mmoja akikatisha kwenda nyuma ambako ndiko mashambulizi yalikokuwa yakisikika sasa. Murphy hakumtaka huyo. Aligeukia ndani kuona kama kulikuwa na bunduki aichukue lakini hata kisu hakikuwepo. Akiwa bado anashangaa, ghafla alitokea adui – kwa ndani – na kurusha risasi, bahati nzuri akamkosa Murphy. Murphy, kama mbayuwayu, aliruka na kusafiri hewani hapohapo akadondoka nyuma ya tangi la gesi karibu na milango ya nje. Alipoona vile, adui alidhani Murphy alidondoka mbali. Alibung’aa asijue la kufanya. Wasiwasi ulipomzidi alishindwa kuvumilia. Alishika bunduki kwa nguvu na kupiga kelele, "Yuko hukuuu!" Halafu akajificha ili Murphy asimwone. Lakini Murphy alikuwa akimwona.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Mlinzi mmoja wa ndani alishtuka aliposikia kishindo cha kitu kudondoka. Aligeuka upesiupesi lakini akaridhika alipokuta ni mwenzake ila akashindwa kuelewa kwa nini mwenzake huyo aanguke. Hata hivyo aliachana na Murphy na kuendelea na lindo lake huku akivuta msokoto mfupi wa bangi. Lakini, yule mlinzi hakutembea hatua nyingi kabla ya kusimama na kujiuliza maswali kichwani. Kwa nini mwenzake huyo atoke nje ambako ndiko alikuwa amepangiwa na ambako ndiko waliambiwa kuwe na ulinzi imara na ndiyo maana wakawekwa saba? Kwa nini aanguke ndani ya ua bila hata ya kumsemesha chochote? Kwa nini hakumpigia redio kwamba alikuwa akiingia ndani ili asiwe na wasiwasi? Alipowaza sana aliamua asiwe na pupa. Aliamua kumfuata mwenzake, aliyekuwa mbele yake, ili amwambie kitu na washirikiane.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita